TUKIO ZIMA LA MKUTANO WA KUFUNGA KAMPENI ZA UDIWANI CHADEMA SOWEPO JIJINI ARUSHA.


Watu wawili wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na kinacho semekana kuwa ni mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo.

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali ya Seliani na Mount Meru.mlipuko huo unasemekana kuwa ulitokea kwenye mkusanyiko wa watu, mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.

Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo baada ya mlipuko huo.

Polisi wapo katika eneo hilo la tukio wakijitahidi kutuliza ghasia lakini inasemekana upo upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wanaojaribu kuwafukuza, hali iliyowalazimu kupiga mabomu ya machozi na kukamata watu kadhaa wakiwemo viongozi wa CHADEMA. 
 
 
VIONGOZI WA CHADEMA WAFIKA TAYARI KUANZA MKUTANO.
 
UMATI WA WATU WALIO HUDHURIA MKUTANO HUO HAPO JANA


 BAADHI YA PICHA NA MATUKIO YA KUSIKITISHA YALIYO TOKEA KATIKA MKUTANO HUO ULIO FANYIKA JANA.









No comments:

Post a Comment