LIST YA WASANII WALIOSHINDA KWENYE KILIMANJARO MUSIC AWARDS NA MATUKOI MENGINE YALIYO JIRI.

Usiku wa jana ulikuwa ni usiku wa furaha sana kwa Mashujaa Band ambao waliongoza kwa kuondoka na tuzo nyingi kuliko wasanii wengne. Mashujaa ambao wanafanya vizuri na wimbo wao wa ''Kidole Risasi'' waliondoka na kura 5 ikiwa ni pamoja na msanii bora wa kiume band Charz Baba, mtunzi bora a mashari ya band Charz Baba, rapper bora wa band Furguson, wimbo bora wa band Risasi Kidole na tuzo ya tano waliichukuwa kupitia category ya band bora ya mwaka huku wakiwatupa kule Twanga Pepeta, Mapacha Watatu na Msondo Ngoma


Wakati huo, upande wa hiphop, Kala Jeremiah aliondoka na tuzo tatu na kuwaacha chini akina Fid Q,Stamina na wengineo, ambapo aliondoka na tuzo ya  msanii bora wa hiphop, mtunzi bora wa mashairi ya hiphop na wimbo bora wa mwaka ''Dear God''Kala ambae ni mwenyeji wa mwanza ambae alikiri kuwa hiyo  ilikuwa kama miujiza kwakwe kuweza kutwaa tuzo zote hizo kwa mpigo


Ommy Dimpoz nae, alisepa na tuzo tatu , wimbo bora wa kushirikiana ''me and you'', video bora ya mwaka ''Baadae'' na wimbo bora wa bongo pop


Mrisho Mpoto ameondoka na tuzo ya wimbo bora wenye vionjo vya asili ''chocheeni kuni''


 Ben pol aliondoka na tuzo ya mtunzi bora wa muziki bongo fleva
 
wengine ni pamoja na Diamond ambae aliondoka na  tuzo ya msanii bora wa kiume na msanii bora wa kiumee bongo fleva. msanii anaechipukia ''Ally Nipishe'', mtayarishaji anaechipukia ''Mensen Selector, wimbo bora wa hiphop ''nasema nao'' Ney wa mitego, wimbo bora wa Zouk/Rhumba ''ni wewe'' Amini, wimbo bora wa Africa mashariki ''Valu valu'' Chameleon, msanii bora wa kike ''Jay Dee,

BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO YALIYO JIRI USIKU HUO
















   

No comments:

Post a Comment