ORIGINAL KOMEDI WASAINI MKATABA MNONO NA KAMPUNI YA NEXUS .



Kundi  la Original Komedi linalovuma kwa vipindi vyake kipitia television imeingia mkataba na kampuni y aNexus Consulting Agency kwa kushirikia  na Rockstar4000. Mkataba huo unaipa nafasi Original Komedi kuwa wasanii wa kwanza wa luninga kufanya kazi na Nexus.


Nexus Consulting Agency imenunua haki zote za usimamizi wa bihashara na viongozi wa kundi hilo la komed ambalo kwa miaka kadhaa sasa limekuwa namba moja katika sanaa ya uchekeshaji. Mkataba huu utakuwa kwa ajili ya kusimamia kipindi cha Orijino Komedi kuweza kuwa namba moja Tanzania pia kupanua utazamwaji wake nje ya mipaka ya Tanzania.Mkataba wa Orijino Komedi na Nexus umetajwa kuwa ni wa kuanzia miaka miwili mmpaka mitano.
Kushirikiana na Orijino Komedi ni kitu muhimu kwa Nexus kwani siku zote imekuwa ikitamani kufanya kazi kwa karibu na kundi hilo na kuthamini kazi zao kutokana ma vipaji vya hali ya juu wanavyo vionyesha kundi hilo alisema mkurugenzi mkuu wa Nexus,Bobby Bharwani. 
Akizungumza kwa niaba ya wenzake muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi,Sekiono David (Seki) na ROCKSTAR4000 Africa,ambapo ameahidi kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kukidhi haja ya soko.Pia Seki alisisitiza kwamba mkataba huu ni mnono sana na utawafanya kufanya kazi zao vizuri sana.
  *ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU*


No comments:

Post a Comment