Rais wa Misri Mohamed Morsi ametangaza kwamba hatajiuzulu licha ya madai kutoka kwa idadi kubwa ya waandamanaji ambao wanamtaka aondoke madarakani.
Rais huyo wa Misri pia alisema jeshi linatoa vitisho vya kutaka kuingilia kati matatizo ya kisiasa nchini humo. Jeshi limeonya kwamba litaweka mwongozo wa hali ya baadae nchini Misri ikiwa tofauti kati ya bwana Morsi na wapinzani wake hazitatatuliwa ifikapo leo Jumatano.
Helikopta ziliruka katika anga ya uwanja wa Tahrir Square, huku waandamanaji wakizishangilia. Maandamano yanazidi kuongezeka huku upinzani ukipata mori baada ya jeshi kumtaka rais Morsi kufikia makubaliano ya kugawana mamlaka nao.Mmoja wao Mohammed Shaaban anasema rais Morsi anaweza kusema lolote kwa watu waliopo Tahrir Square, lakini wao ndiyo wenye maamuzi kwa sasa.
Wachambuzi wa maswala ya kisiasa wanasema waandamanaji wanahisi haya ni mapinduzi ya pili na kwamba walichokidai Januari mwaka wa 2011, ikiwa ni pamoja na mahitaji ya kimsingi, uhuru na haki bado hayajatekelezwa.
Nazo Uingereza na Ujerumani zimekariri wasiwasi wao kwa rais wa Marekani Barack Obama juu ya mzozo huo hapo jana na kuhimiza kuwepo kwa suluhisho la amani.
No comments:
Post a Comment