Rais wa Marekani akicheza muziki wa band wakati alipotua uwanjani
Obama
akiwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete.Rais wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Tanzania
leo Jumatatu kwa ziara ya siku mbili, ikiwa ni kituo chake cha mwisho cha ziara
yake barani Afrika akitokea nchini Afrika Kusini.
Obama
ambaye ameambatana na mkewe Michelle Obama amepokelewa na mwenyeji wake rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Salma Kikwete katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kisha kuelekea Ikulu ya rais. NA
MPEKUZI
Rais
Obama na mwenyeji wake wanatarajiwa kufanya mazungumzo ya pamoja na kisha Obama
atafanya mazungumzo na waandishi wa habari kabla ya kushiriki dhifa ya pamoja
na viongozi mbalimbali wa serikali hapo baadaye Ikulu jijini Dar es Salaam.
Aidha
hapo kesho Obama atatembelea kituo cha umeme cha Ubungo , baada ya kuahidi
kutoa dola za Marekani bilioni saba kusaidia mradi wa umeme Barani Afrika.
Mpango
huo wa serikali ya Marekani utazinduliwa kwanza katika nchi za Ethiopia, Ghana,
Kenya, Liberia, Nigeria na Tanzania ambazo wananchi wake wanakumbwa na matatizo
ya upatikanaji wa umeme.
Karibu
Barack Obama kanga pamoja na vitenge waliova wananchi wa waTanzania
Katika
ziara yake Barani Afrika iliyoanzia nchini Senegal, Afrika kusini na hatimaye
nchini Tanzania Obama amekuwa akisisitiza suala la demokrasia ambapo ameeleza
kuwa Afrika itakuwa na mustakabali mzuri kwa kuwa na viongozi wanaopambana
kuhakikisha raia wao wanakuwa na maisha bora.
Katika
ziara yake nchini Afrika Kusini , Obama hakusita kusifu jitihada za kiongozi wa
zamani na baba wa taifa hilo Nelson Mandela ambaye ameeleza kuwa jitihada zake
za ukombozi kwa raia wa taifa hilo zilimsukuma kuingia katika siasa na hatimaye
kuwa rais wa kwanza mweusi nchini Marekani
No comments:
Post a Comment