Pamoja na kuwa wana ushahidi wa Picha, Mikanda ya Video
inayoonyesha jinsi Polisi walivyoshiriki kulipua bomu la Arusha, Chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema wamesema hawapo tayari kupokea pesa
zilizotengwa na serikali kwa ajili ya mtu atakayetoa taarifa kuhusu waliohusika
na mlipuko wa Arusha.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisi za Chama hicho
Makao Makuu, Msemaji wa Chama hicho John Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo
alisema “hata kama bado hatujakaa kama Chama kuafikiana suala hili, hizo pesa
kuzichukua ni ufisadi tu, matumizi mabaya ya pesa, serikali imepata wapi pesa
za kulipa milioni mia kwa watoa taarifa wakati haijawahi hata kutoa rambirambi
kwa mjane wa Daudi Mwangosi, licha ya kwamba Polisi walihusika kwa asilimia
zote katika kuua, hatuwezi kuhuchukua hizo pesa.
Kwanza ifahamike kwamba serikali imeamua kutenga hilo fungu
ili kuhalalisha matumi mabovu ili kuhalalisha ulaji wa pesa, ije iseme
tuliwalipa watoa taarifa, huu ni uongo, na serikali inapokuwa inadanganya raia
wake inakosa uadilifu wa kuendelea kutawala.
Suala la Arusha ni tete, serikali imekuwa ikisema uongo
hapa na pale, ndio maana hata Mizengo Pinda tangu aseme uongo suala hilo
halijawahi kuzungumzwa Bungeni, Spika analipiga danadana kila mara.
Aidha katika mkutano huo, Mnyika amelitaka jeshi la polisi
liwaachie vijana watatu wanaoteswa na Jeshi hilo ili kuwalazimisha kutoa
mikanda waliyorekodi ambayo Mbowe anasema wanayo inayoonyesha jinsi Polisi
walivyolipua bomu, kuwapiga risasi watu waliotaka kumkamata aliyelipua bomu, na
gari ya polisi iliyomtorosha mtu aliyerusha bomu. Jeshi la Polisi mkoani Arusha
linawashikilia vijana watatu makada wa Chadema, ili liweze kupata mikanda hiyo
kwa nguvu bila kutumia njia za kuwaomba.
No comments:
Post a Comment